Ijumaa 2 Oktoba 2026 - 11:35
Kondoa Yatikisa kwa Sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Viongozi na Waumini Wakutana

Hawza/ Siku ya jana Alhamisi Oktoba 1, 2026, Kondoa Mjini lilishuhudia hafla kubwa ya kuadhimisha Maulidi ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w.), iliyowakutanisha viongozi wa dini, masheikh, wanazuoni na waumini kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Sheikh Abdullatif Swa’leh na kuhudhuriwa na viongozi na masheikh mbalimbali, akiwemo Sayyid Edarusi pamoja na jopo lake kutoka Kenya; Sheikh Abdurazaki Amiri na jopo lake kutoka Arusha; Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayyid Shuhadaa, Sheikh Maulid Sombi, kutoka Arusha; pamoja na Sheikh wa Mkoa wa TIC Dar es Salaam, Sheikh Saidi Othman.

Aidha, hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mwakilishi wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma kutoka BAKWATA, pamoja na wageni wengine mbalimbali kutoka maeneo tofauti, ambao waliungana na waumini wa Kondoa katika kuadhimisha kumbukumbu tukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), tukio linalobeba ujumbe mkubwa wa kiroho na kijamii kwa Waislamu.

Katika maadhimisho hayo, wahudhuriaji walipata fursa ya kusikiliza mawaidha na jumbe mbalimbali za kidini zilizolenga kuwakumbusha Waislamu umuhimu wa kuufuata mwenendo na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika maisha yao ya kila siku.

Miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa ni umuhimu wa kuijenga jamii yenye amani, upendo, umoja, mshikamano, huruma na maadili mema, kwa kuiga mwenendo wa Mtume (s.a.w.w.) ambaye alileta ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu katika njia ya haki, uadilifu na utu.

Hafla hiyo ya Maulidi imekuwa pia fursa ya kuimarisha udugu na mshikamano miongoni mwa Waislamu, huku ikitoa nafasi kwa viongozi wa dini na waumini kukutana, kubadilishana nasaha na kuhuisha mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika jamii.

Kondoa Yatikisa kwa Sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Viongozi na Waumini Wakutana Katika Kumbukumbu ya Kuzaliwa Mbora wa Viumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha